Polisi wawili wa Kenya wauawa katika mlipuko wa barabarani
2023-09-04 08:36:50| CRI

Askari polisi wasiopungua wawili wa Kenya wameuawa katika mlipuko uliotokea kando ya barabara Jumapili iliyopita huko kaskazini mashariki mwa Kenya huku wengine sita wakijeruhiwa.

Polisi ya Kenya imesema askari polisi hao kutoka kikosi cha mwitikio wa haraka walikuwa wakifanya doria kutoka Arabia hadi mji wa Mandera karibu na mpaka na Somalia walipokanyaga bomu la kienyeji lililotegwa kando ya barabara. Sasa majeruhi wamepelekwa hospitali, wawili kati yao wako kwenye hali mbaya.