Kampuni ya Uber yazindua pikipiki zinazotumia umeme nchini Kenya
2023-09-04 14:22:00| cri

Kampuni ya magari ya kukodi ya Uber imezindua huduma ya pikipiki za kukodi zinazotumia umeme nchini Kenya, ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na huduma hiyo.

Kampuni hiyo imesema, pikipiki hizo zilizopewa jina la Boda ya Umeme, itahusisha pikipiki 3,000 ndani ya miezi sita, na madereva watashuhudia kushuka kwa gharama za matumizi kwa asilimia 30 hadi 35, na kwa upande wa watumiaji wa usafiri huo, watashuhudia malipo ya chini ya asilimia 15 mpaka 20 ya gharama wanazotumia kwa usafiri wa kawaida wa Uber.