Bunge la Afrika Kusini kufanya uchunguzi kuhusu ajali ya moto Johannesburg
2023-09-04 08:18:12| CRI

Bunge la Afrika Kusini limesema litafanya uchunguzi kuhusu ajali ya moto iliyotokea alhamisi kwenye jengo la ghorofa tano mjini Johannesburg na kusababisha vifo vya watu 77.

Taarifa iliyotolewa na bunge inasema maofisa waandamizi wa bunge wamesema bunge litafanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo ambayo pia imeleta madhara kadhaa na kufanya watu 300 kupoteza makazi.

Taarifa pia imesema hali ya sasa ya majengo “yaliyovamiwa” inatakiwa kuchunguzwa. Majengo ya namna hiyo ni majengo ya zamani yaliyotelekezwa na wamiliki au mamlaka za mji, na zimejaa watu wanaolipa kodi kwa magenge ya uhalifu. Mara nyingi majengo hayo hayana maji, maliwato au umeme uliounganishwa kihalali.