Rais Xi Jinping apongeza Maonesho ya Kimataifa ya Akili Bandia
2023-09-04 23:15:47| cri

Xi Jinping wa China ametuma salama za pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Akili Bandia ya China ya mwaka 2023.

Kwenye salamu zake, rais Xi ameamesema, hivi sasa teknolojia mpya kama vile Internet, data kubwa, kompyuta ya wingu, akili bandia, na blockchain zimepata maendeleo makubwa, na kubadilisha sana mambo ya kimataifa, njia za ugavi wa rasilimali, maendeleo ya viwanda na  maisha ya watu. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani ili kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja katika masuala ya mtandao, na kuanzisha maisha bora zaidi katika siku zijazo.