Uzalishaji wa mafuta kwa siku nchini Libya wafikia mapipa milioni 1.2
2023-09-04 08:35:14| CRI

Shirika la Taifa la Mafuta la Libya (NOC) limesema uzalishaji wa mafuta kwa siku nchini Libya kwa sasa umefikia mapipa milioni 1.204.

Shirika hilo lilimetoa takwimu hizo kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, wakati uzalishaji wa kila siku wa mafuta ghafi mepesi ni mapipa 50,000.

Mafuta na gesi ndio chanzo kikuu cha mapato ya Libya. Hata hivyo katika miaka ya karibuni sekta hiyo imesumbuliwa kutokana na mgogoro ya kijeshi na kufungwa kwa maeneo ya mafuta na bandari.