Algeria yafanya sherehe ya kuaga timu ya madaktari ya China
2023-09-04 08:11:27| CRI

Sherehe ya kuaga timu ya 27 ya madaktari ya China ilifanyika jana Jumapili katika makao makuu ya Wizara ya Afya ya Algeria mjini Algiers.

Madaktari wa timu hiyo walitunukiwa vyeti vya heshima na serikali ya Algeria kwenye sherehe hiyo, iliyohudhuriwa na Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bwana Abdelhak Saihi, balozi wa China nchini humo Li Jian na maofisa wengine na wataalamu wa afya.

Bwana Saihi ameshukuru juhudi za bila kusita na msaada muhimu uliotolewa na timu ya madaktari wa China kwa Algeria, akisema huduma zao na ujuzi walioutoa vimeimarisha urafiki na uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye hafla hiyo, Balozi Li amewapongeza madaktari wa timu hiyo kwa kukamilisha majukumu yao nchini Algeria na kutunukiwa vyeti vya heshima, ambavyo pia ni ushahidi wa urafiki imara kati ya nchi hizo mbili.