Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika ya Kati yaisimamisha uanachama Gabon baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo
2023-09-05 09:18:14| CRI

Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati imeamua kuisimamisha uanachama Gabon baada ya mapinduzi ya kijeshi kutokea nchini humo wiki iliyopita.

Viongozi wa jumuiya hiyo wametoa uamuzi huo kwenye mkutano uliofanyika jana wakilaani matumizi ya nguvu katika kutatua mgogoro wa kisiasa na kutaka kurejeshwa haraka kwa utaratibu wa kikatiba nchini Gabon.

Wanajeshi waliofanya mapinduzi wametwaa madaraka nchini humo wiki iliyopita ambapo walimweka rais Ali Bongo kizuizini nyumbani kwake, na kumteua kiongozi mpya, baada ya rais Bongo kutangazwa mshindi katika duru ya tatu ya uchaguzi mkuu tarehe 26 Agosti.