UM na washirika wake waomba dola bilioni moja za kimarekani kusaidia wakimbizi nchini Sudan
2023-09-05 08:46:34| CRI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), na mashirika 64 ya kibinadamu na kiraia yameomba kupatiwa dola bilioni moja za kimarekani ili kutoa misaada na ulinzi kwa watu zaidi ya milioni 1.8 waliokimbia mgogoro nchini Sudan.

Mkurugenzi wa UNHCR eneo la Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu, ambaye pia ni mratibu wa kikanda wa wakimbizi kwa Sudan, Mamadou Dian Balde amesema msukosuko huo umezusha mahitaji ya haraka ya msaada wa kibinadamu, wakati watu wanaokimbilia maeneo ya mbali wanakabiliwa na mazingira magumu ya maisha kutokana na ukosefu wa huduma, miundombinu hafifu na ufikiaji mdogo.

Shirika hilo limesema ombi hilo la fedha limetolewa kwenye msingi wa makadirio yaliyorekebishwa, ambayo yanakadiria ongezeko maradufu kutoka yale yaliyotolewa mwezi Mei.