Kenya yazindua mpango wa ufadhili wa hali ya hewa wa Dola za Kimarekani milioni 50
2023-09-05 23:39:19| cri

Kenya jana ilizindua mpango wa ufadhili wa hali ya hewa wa shilingi bilioni 7.37 (kama dola milioni 50.6) kwa kaunti za nchini humo, huku ikilenga kuimarisha juhudi za kukabiliana na hali hiyo katika ngazi ya mashina.

Akizindua Ruzuku ya Kaunti ya Kustahimili Hali ya Hewa (CCRI) iliyotolewa chini ya Mpango wa Ufadhili wa Hali ya Hewa kwa Kaunti za Afrika Mashariki (FLLoCA) katika Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, Rais William Ruto wa nchi hiyo amesema fedha hizo zitasaidia kaunti za vijijini kutunga na kutekeleza mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia amesema, fedha hizo zitasaidia kaunti kukabiliana na hatari zinazotambuliwa na jamii kama vile katika kilimo, maji na usimamizi wa maliasili.