Maofisa wa Afrika wasema mageuzi ya kijani yanaendelea vema licha ya hali tete ya dunia
2023-09-05 14:40:21| cri

Maofisa wa ngazi ya juu wa Afrika wamesema, mageuzi ya kijani barani Afrika yako katika mwelekeo sahihi licha ya hali tete ya dunia inayohusishwa na mvutano wa siasa za kijiografia na ufufukaji wa taratibu kutoka katika janga la COVID-19.

Akizungumza kabla ya Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa Afrika mwaka 2023 mjini Nairobi, Kenya, Kamishna wa Idara ya Uchumi wa Vijijini na Kilimo katika Kamati ya Umoja wa Afrika Josefa Sacko amesema, haja ya bara hilo ya kupunguza uchafuzi wa hewa na ukuaji jumuisho imeshika kasi kutokana na kuungwa mkono kisiasa, ufadhili katika uvumbuzi, na utekelezaji wa sera rafiki.

Kenya, kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), imeandaa mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa Afrika unaofanyika mjini Nairobi kuanzia jana jumatatu hadi kesho jumatano, ukiwa na kaulimbiu ya “Kuchochea Ukuaji wa Kijani na Suluhisho la Ufadhili wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa Afrika na Dunia.”