Iran iko tayari kuhamisha uzoefu kwa nchi rafiki za Afrika
2023-09-05 09:19:58| CRI

Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Iran iko tayari kuhamishia uzoefu wa mafanikio yake kwa nchi rafiki, hasa zile za Afrika.

Alisema hayo wakati alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Bw. Olivia Rouamba aliyeko ziarani nchini Iran, ambapo pia walijadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Raisi amesifu uhusiano mzuri wa Iran na nchi nyingi za Afrika baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, na amezisifu nchi hizo kwa kupambana na ukoloni na ugaidi.

Bw. Rouamba amesema nchi za Afrika ikiwemo Burkina Faso zinapata msukumo kutokana na mapinduzi ya Kiislamu ya Iran dhidi ya mfumo wa umwamba duniani.