Makampuni ya dawa ya China yachunguza soko barani Afrika, Mashariki ya Kati katika maonesho ya sekta ya dawa ya Cairo
2023-09-05 08:43:42| CRI

Makampuni ya dawa ya China yameshiriki kwenye maonesho ya sekta ya dawa ya Misri Pharmaconex 2023 yanayoendelea kufanyika mjini Cairo, ili kuchunguza fursa za biashara nchini Misri, Afrika na Mashariki ya Kati.

Waratibu wa maonesho hayo wamesema maonyesho hayo ya siku tatu yaliyoanza jana yamekusanya makampuni ya dawa kutoka Misri, China, India, Marekani, Italia, Ufaransa, Ubelgiji, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Maofisa wa kampuni za dawa za China wamesema wanapenda kutangaza bidhaa zao nchini Misri na katika maeneo mengine ya Mashariki ya Kati na wanatarajia kujenga uhusiano na wenzao wa Misri kupitia maonyesho hayo.

Mwenyekiti wa kampuni ya dawa ya China Coben Pharma, Fang Zhenrong, amesema soko la Misri linakua na wanatarajia kuongeza ushirikiano wa kibiashara kati ya makampuni ya China na Misri kwani nchi hizo mbili zimekuwa zikiimarisha uhusiano wao chini ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.