Rais mteule wa Zimbabwe aapishwa kuwa rais kwa kipindi cha pili
2023-09-05 09:04:23| CRI

Rais mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa kwa kipindi cha pili cha miaka mitano madarakani katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa kikanda na nchi za nje. Bwana Mnangagwa ameapishwa baada ya kushinda kwa kupata asilimia 52.6 ya kura zote katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita.

Kabla ya hapo mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa wa chama kikuu cha upinzani cha CCC aliyepata asilimia 44 ya kura alikataa matokeo ya uchaguzi na kutoa mwito wa kufanya upya uchaguzi, kwa madai ya kuwepo kwa dosari kwenye uchaguzi.

Habari nyingine zinasema, kutokana na mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, mjumbe maalumu wa Rais Xi Jinping wa China Bw. Zhou Qiang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Mnangagwa huko Harare.

Rais Mnangagwa amekutana na Bw. Zhou ambaye amewasilisha pongezi na matumaini mema kutoka Rais Xi.