China kuchukua jukumu la upatanishi katika mgogoro wa Niger
2023-09-06 23:04:55| cri

Balozi wa China nchini Niger, Jiang Feng, amesema nchi yake inakusudia kuchukua jukumu la usuluhishi katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Mwanadiplomasia huyo ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanya Jumatatu Septemba 4, 2023 kwenye televisheni ya taifa ya Niger, mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ali Mahaman Lamine Zeine, aliyeteuliwa na wanajeshi kushika wadhifa huo. Serikali ya China inakusudia kuchukua jukumu la kuwa mpatanishi, ili kutafuta suluhisho la kisiasa la mzozo huu wa Niger.

Ameongeza kuwa China inafuata misingi na kanuni ya kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, hivyo amezihimiza nchi za Afrika, kutatua matatizo yao kwa njia ya amani kupitia meza za mazungumzo.