Wajasiriamali 10 wa Afrika kuwania tuzo ya wafanyabiashara hodari wa Afrika 2023
2023-09-06 09:01:46| CRI

Jumla ya washindi 10 wamechaguliwa kugombea tuzo za mwaka huu za Wafanyabiashara hodari Afrika (ABH) zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka huu mjini Kigali, ambapo washindi wanatarajiwa kujipatia zawadi ya fedha.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa tuzo hiyo inayofadhiliwa na mfuko wa Jack Ma, wamesema watu hao wanaoingia fainali walichaguliwa kupitia mchakato mkali kwenye nusu fainali, iliyofanyika ijumaa na jumamosi mjini Kigali.

Watu 10 walioingia fainali wanatarajiwa kugombea dola za Marekani milioni 1.5, kwenye fainali itakayofanyika Novemba 23-24.

Washindi hao wanatoka Benin, Misri, Ghana, Kenya, Morocco, Nigeria, Rwanda na Afrika Kusini, na walichaguliwa kutoka kwa zaidi ya waombaji 27,000 katika nchi 54 za Afrika, wakitoka kwenye sekta za kilimo, elimu na mafunzo, nishati, huduma za kifedha, afya, viwanda na biashara ya rejareja.