Mwenyekiti mpya wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Dennis Francis, ametangaza kufunguliwa kwa kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Kwenye hotuba iliyotolewa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres na kusomwa na naibu wake Bibi Amina Mohammed, Katibu Mkuu ameonya kuhusu dunia yenye changamoto kubwa na mgawanyiko unaoleta changamoto kwa Umoja wa Mataifa.
Bw. Guterres amesema licha ya changamoto kubwa za kimataifa, huu si wakati wa kukata tamaa, bali ni wakati wa kuchukua hatua, kwa ajili ya amani na haki za binadamu; hatua ya kuokoa Malengo ya Maendeleo Endelevu na kukabiliana na tishio lililopo la mabadiliko ya tabia nchi, na kuchukua hatua za kuongeza nafasi za ajira na kupanua fursa za kiuchumi.
Habari pia zinasema Sudan pia inashiriki kwenye mkutano huo, na imetuma ujumbe unaoongozwa na mwenyekiti wa baraza la mpito la utawala na mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan.