Wapiganaji 53 wauawa kaskazini mwa Burkina Faso
2023-09-06 09:20:33| CRI

Jeshi la Burkina Faso limesema kupitia taarifa kuwa wapiganaji 53 wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa katika mapigano makali na magaidi yaliyotokea jumatatu kaskazini mwa Burkina Faso.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makumi ya magaidi waliangamizwa kwenye mapigano katika mji wa Koumbri jimboni Yatenga, na operesheni bado inaendelea.

Tangu mwaka 2015, ukosefu wa usalama nchini Burkina Faso umesababisha vifo vya watu wengi na wengine maelfu wamepotea makazi yao.