Maofisa wa Afrika wajadili njia za kutatua upungufu wa wahudumu wa afya
2023-09-06 08:38:47| CRI

Maofisa wa afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamekutana mjini Kigali, Rwanda Jumatatu Septemba 4 kujadili changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za afya barani Afrika, haswa njia za kutatua upungufu wa madaktari.

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Shirikisho la Mabaraza ya Kimatibabu la Afrika (AMCOA), ambalo linaleta pamoja mamlaka za matibabu barani humo.

Shirika la Afya Duniani WHO limependekeza kiwango cha chini cha kuwepo kwa wahudumu wa afya 4.45 kwa kila watu elfu moja ili kuweza kutoa huduma muhimu za afya kwa wote, lakini nchi nyingi za Afrika zimeshindwa kufikia kiwango hicho.