Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameamua kurefusha muda kikosi cha jumuiya hiyo kilichotumwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kurejesha utaratibu na usalama kwa miezi mitatu zaidi.
Uamuzi huo umetangazwa kupitia taarifa iliyotolewa kufuatia Mkutano Maalumu wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jumanne mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wamekubali kwa kauli moja kurefusha muda wa kikosi cha kikanda nchini DRC hadi kufikia Desemba 8 mwaka huu.