Kenya yaondoa vizuizi vya viza kwa wasafiri kutoka DR Congo
2023-09-07 11:18:07| cri

Kenya imeondoa masharti ya viza kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kwa hivyo, wenye hati za kusafiria za kitaifa za DR Congo sasa wanaweza kusafiri hadi Kenya bila kuhitaji viza.

Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Uhamiaji na Raia, Evelyn Cheluget alisema kuwa msamaha huo unazingatia “kanuni za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu kusafiri huru kwa watu ndani ya nchi wanachama. Rais William Ruto pia alitoa agizo hilo Julai 2023.