Kuinuka kwa uhusiano kati ya China Benin kwaonesha dhana ya ukweli, uhalisi, urafiki na udhati ya China kwa Afrika
2023-09-07 15:12:57| CRI

Rais wa China Xi Jinping hivi karibuni alifanya mazungumzo na Rais wa Benin Patrice Talon, ambaye alikuwa ziarani nchini China, na kutangaza kuanzishwa kwa ushirikiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Kuinuka kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kutasukuma mbele zaidi ushirikiano kati ya China na Benin na China na Afrika, na ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja katika enzi mpya.

Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao wawili walishuhudia kusainiwa kwa makubaliano kadhaa ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za kuimarisha ujenzi wa pamoja wa "Ukanda na Barabara", maendeleo ya kijani, uchumi wa kidijitali, kilimo na chakula, na huduma za afya.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo inasema, pande hizo mbili zitahimiza kuunganisha ujenzi wa pamoja wa mapendekezo ya China ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Maendeleo ya Kimataifa, na mipango ya Benin ya “Mpango wa Maendeleo wa Kitaifa wa Mwaka 2018-2025” na “Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa mwaka 2021-2026”.

Huu ni mwaka wa 10 tangu Rais Xi kutoa Dhana ya Ukweli, Uhalisi, Urafiki na Udhati. Katika mwongo uliopita, China imekuwa ikifuata dhana hiyo wakati inapofanya ushirikiano na nchi za Afrika, na ushirikiano huo umekuwa mfano wa kuigwa kwa uhusiano wa kimataifa.

Katika mazungumzo na Rais Talon, rais Xi amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba China inaunga mkono Afrika kuwa moja ya nguzo muhimu za maendeleo ya mambo ya siasa, uchumi na utamaduni duniani. Amesema China pia inapenda kutoa fursa mpya kwa Afrika kutokana na maendeleo mapya ya China, na kushirikiana na Afrika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mikutano ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuhimiza ushirikiano wa kina wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Mpango wa Maendeleo ya Kimataifa, “Ajenda ya 2063” ya Umoja wa Afrika na mikakati mingine ya maendeleo ya nchi za Afrika, na kuzisaidia nchi za Afrika katika kutimiza ufufuaji wa uchumi na maendeleo endelevu.

China daima imekuwa ikiiunga mkono Afrika kwa dhati, na iko tayari kuwa mshirika wake katika mchakato wa kutimiza mambo ya kisasa barani Afrika.

Katika mazungumzo ya viongozi wa China na Afrika yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti wakati wa mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS, Rais Xi alitangaza kuwa China imezindua “Pendekezo la Kuunga Mkono Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika”, “Mpango wa Kuisaidia Afrika kuwa na Kilimo cha Kisasa”, na “Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Kufundisha Watu wenye Vipaji.”

Katika siku zijazo, China itaendelea kufuata Dhana ya Ukweli, Uhalisi, Urafiki na Udhati, kuchukua hatua za kivitendo kuisaidia Afrika kujiendeleza, na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja katika enzi mpya.