Saudi Arabia na Uganda zasaini makubaliano ya mkopo wa dola milioni 30
2023-09-07 09:12:53| CRI

Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia (SFD) jana ulisaini makubaliano ya mkopo wa maendeleo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 30 na Uganda, ili kufadhili mradi wa taasisi ya moyo ya nchi hiyo.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha sekta ya afya ya Uganda na kutoa msaada kwa Mpango wake wa tatu wa Maendeleo wa Kitaifa wa miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2024/25, ambao unaainisha mwelekeo wa kimkakati wa muda wa kati, vipaumbele vya maendeleo na mikakati ya utekelezaji, na kuongeza tija na ustawi wa jamii.

Mradi huo unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu elfu 62, kutoa nafasi za ajira katika sekta ya matibabu, na kuchochea ukuaji wa uchumi.