Umoja wa Afrika wafikiria kuweka mkakati wa kijani wa madini ili kuhimiza ukuaji endelevu
2023-09-07 14:42:59| cri

Umoja wa Afrika Jumanne ulitangaza mkakati wa kijani wa madini barani humo, ili kutumia raslimali kwa ajili ya kuhimiza mapato na ukuaji endelevu wa nchi zenye madini.

Marit Kitaw, mkurugenzi wa muda wa Kituo cha Maendeleo ya Madini cha Afrika, ambayo ni shirika maalum la Umoja wa Afrika linalojishughulisha na madini kwa maendeleo endelevu ya Afrika, alisema mpango huo wa kimkakati unalenga kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kwa kufuata kanuni za Dira ya viwanda vya madini barani Afrika.

“Mkakati huo unalenga kubadilisha minyororo ya thamani ya madini kwa kutumia raslimali za madini kutengeneza bidhaa za lazima barani humo, na kusitisha usafirishaji nje wa malighafi. ” Kitaw alisema katika mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa Afrika unaofanyika huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya.