Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani anayehusika na masuala ya hali ya hewa John Kerry amesema kuwa Marekani aliapa kwamba labda Marekani iwe imelaaniwa ndio italipa fidia ya hali ya hewa kwa nchi zinazoendelea.
Licha ya kuwa nchi yake ni miongoni mwa nchi zinazotoa hewa chafuzi duniani, alisisitiza kauli yake aliyoitoa katika kikao cha bunge Julai mwaka huu kwamba kwa hali yoyote ile nchi yake haitalazimika kulipa fidia ya hali ya hewa.
Katika mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika, alisema licha ya kuwa anafahamu Marekani ni miongoni mwa wachafuzi wakubwa wa mazingira, uchumi wa nchi zote duniani uko katika hali hiyo hiyo ya taabu linapokuja suala la mabadiliko ya tabianchi.