Mkutano wa kilele wa tabianchi wa Afrika wapitisha Azimio la Nairobi
2023-09-07 09:19:10| CRI

Mkutano wa kwanza wa kilele wa Afrika kuhusu tabianchi umefungwa Septemba 6 mjini Nairobi na kupitisha Azimio la Nairobi, likitoa wito kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea kuungana mkono katika kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kuzitaka nchi zilizoendelea zitekeleze ahadi za kutoa misaada husika ya kifedha na kiufundi.

Viongozi wa nchi za Afrika wamependekeza jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati endelevu kutoka megawati 56,000 za mwaka 2022 hadi megawati 300,000 ifikapo mwaka 2030.

Washiriki wengi wametoa wito kwenye mkutano huo kwamba mfumo wa fedha wa kimataifa ungefanyiwa mageuzi na kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuunga mkono taasisi za kifedha za Afrika na kusaidia nchi zinazoendelea kuboresha hali zao za kiuchumi ili ziweze kukabiliana vizuri zaidi na mabadiliko ya tabianchi.