Mlipuko wa kipindupindu watokea magharibi mwa Burundi
2023-09-07 08:33:17| CRI

Wizara ya Afya ya Burundi imesema maambukizi 15 mapya ya ugonjwa wa kipindupindu yameripotiwa magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Umma na Udhibiti wa UKIMWI ya Burundi Polycarpe Ndayizeye amesema, jumla ya wagonjwa 30 wanapatiwa matibabu katika hospitali huko Bujumbura, Gatumba na Rugombo. Amezitaka mamlaka za usimamizi, wakazi wote kwenye maeneo yaliyoathirika na wadau wote kutoa mchango kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Uhaba wa maji unaripotiwa mara kwa mara magharibi mwa Burundi, hasa kwenye msimu wa kiangazi kuanzia Mei hadi Septemba, hali inayosababisha milipuko ya kipindupindu karibu kila mwaka.