Waziri Mkuu wa China ahudhuria Mkutano wa 18 wa Kilele wa Asia Mashariki
2023-09-08 08:51:58| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang amehudhuria Mkutano wa 18 wa Kilele wa Asia Mashariki huko Jarkarta, Indonesia.

Bw. Li Qiang amesema katika miongo kadhaa iliyopita, Asia Mashariki imetumia vizuri fursa za maendeleo kwenye mkondo wa mafungamano ya kiuchumi duniani, kufuata kithabiti njia sahihi ya kujiendeleza kwa uwazi na kushirikiana kwa kunufaishana, na imekuwa injini muhimu ya kuhimiza maendeleo ya dunia.

Bw. Li Qiang ameainisha kuwa mkutano wa kilele wa Asia Mashariki unapaswa kutoa mchango mkubwa zaidi katika kudumisha utulivu na ustawi kwenye kanda hiyo.

Bw. Li Qiang amesema, China na nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) zinajitahidi kusukuma mbele mazungumzo kuhusu Kanuni za Mienendo katika Bahari ya Kusini. Anatumai kuwa nchi zisizo za kanda hiyo zitaheshimu kikamilifu juhudi zinazofanywa na nchi za kanda hiyo kwa ajili ya kuandaa kanuni za bahari ya kusini na kulinda amani na utulivu kwenye eneo hilo.