Idara ya uhamiaji ya Tanzania yaishukuru China kwa kutoa vifaa vya elimu
2023-09-08 23:41:49| cri

Idara ya uhamiaji ya Tanzania Jumatano iliushukuru ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutoa vifaa vya elimu kwa Chuo cha Uhamiaji (TRITA) kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro Tanzania.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian kwa kamishna mkuu wa uhamiaji nchini Tanzania, Anna Makakala, katika ofisi ya huduma za uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Makakala alisema, vifaa vya elimu vitaboresha huduma za Idara ya Uhamiaji. Alibainisha kuwa ana matarajio makubwa kwamba ushirikiano kati ya Idara ya Uhamiaji ya Tanzania na Ubalozi wa China nchini Tanzania utaendelea kwa muda mrefu.