Kikundi cha kumi cha madaktari wa China chatunukiwa vyeti nchini Sudan Kusini
2023-09-08 09:05:36| CRI

Sudan Kusini na ubalozi wa China wamekitunuku vyeti kikundi cha kumi wa madaktari wa China kinachomaliza muda wake nchini Sudan Kusini, ili kutambua mchango wao katika kutoa huduma bora za matibabu kwa watu wa nchi hiyo.

Hafla ya kuwatunuku vyeti ilifanyika kwenye Ubalozi wa China mjini Juba, ambapo ofisa mwandamizi wa wizara ya afya ya Sudan Kusini Bw. Atem Nathan Nyuon, aliwapongeza madaktari hao kwa mchango mkubwa ulioleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini humo tangu mwaka 2012.

Mkuu wa Hospitali ya Mafunzo ya Juba Bw. Anthony Lupai Simon, amesema madaktari hao wa China sio kama tu wamekaa kwenye hospitali hiyo tu, bali pia wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo ya mbali na magumu kufikiwa kama vile Paloch, Panyagor na Rumbek.