IGAD yatoa mwito wa kufanya mazungumzo shirikishi kumaliza mapigano nchini Sudan
2023-09-08 09:16:32| CRI

Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki IGAD imesisitiza mwito wake wa utatuzi wa amani wa mgogoro uliodumu kwa miezi mitano nchini Sudan.

Viongozi wa kundi la pande nne la IGAD ikiwa ni pamoja na Kenya, Ethiopia, Sudan Kusini na Djibouti, wamekutana mjini Nairobi, na kuihimiza IGAD yenye nchi wanachama wanane na Umoja wa Afrika, kufanya juhudi za pamoja na nchi jirani za Sudan na pande husika za kimataifa kuunga mkono mchakato wa amani.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na marais wa Kenya, Djibouti na Sudan Kusini na mjumbe wa Ethiopia, umeitaka IGAD na Umoja wa Afrika kuweka ajenda na kuthibitisha washiriki na mambo mengine husika katika uungaji mkono wa mazungumzo ya kisiasa yanayoweka bayana mchakato wa kisiasa unaoongozwa na watu wa Sudan.