Rais wa China awatembelea wakazi wa Shangzhi mkoani Heilongjiang waliokumbwa na mafuriko
2023-09-08 15:20:06| cri

Rais Xi Jinping wa China jana mchana alikwenda kijiji cha Longwangmiao kilichoko katika tarafa ya Laojieji, kaunti ya Shangzhi mjini Harbin mkoani Heilongjiang, sehemu ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa.

Rais Xi alikagua uharibifu uliosababishwa na mafuriko hayo katika mashamba ya mpunga, na kuangalia nyumba zilizoharibiwa na ukarabati wa miundombinu kijijini, pia aliwatembelea watu wa huko na kufuatilia hali ya maafa na maeneo ya muda wanayoishi. Rais Xi amewataka wawe na nia imara katika kushinda changamoto hiyo, na kurejea kwenye shughuli zao na maisha ya kawaida haraka iwezekanavyo na kupata maisha bora zaidi.