Watu 12 Wafariki Katika Ajali ya Barabarani eneo la Ndii Voi Kando ya Barabara kuu ya Nairobi-Mombasa
2023-09-08 14:45:44| cri

Mamlaka mjini Voi zilithibitisha kuwa takriban watu kumi na wawili walifariki katika ajali mbaya iliyohusisha matatu na lori katika eneo la Ndii karibu na Voi kando ya barabara kuu ya Nairobi-Mombasa jana Alhamisi.

Mkuu wa polisi wa Voi Bernstein Shari alisema gari hilo la matatu lililokuwa likielekea Mombasa na kuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Genesis Shuttle liligongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya watu kadhaa papo hapo.

Alisema watu watatu waliopata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea saa kumi na dakika ishirini alfajiri walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Moi kaunti ya Voi.