Mwenyekiti wa AU aishukuru China kwa kuiunga mkono Umoja huo kujiunga na G20
2023-09-11 10:42:27| CRI

Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Comoro Azali Assoumani ameishukuru China kwa kuiunga mkono Umoja huo kujiunga na Kundi la Nchi 20 (G20), na kusema nchi za kusini zitashirikiana na nchi nyingine kuhimiza ushirikiano mzuri zaidi wa kimataifa, ili kukabiliana na changamoto za siku zijazo.

Umoja wa Afrika ulikuwa mwanachama rasmi wa G20 tarehe 9 kwenye Mkutano wa 18 wa Kilele wa Viongozi wa G20 uliofanyika mjini New Delhi nchi India.

Assoumani amesema uhusiano wa kushirikiana kati ya China na Afrika umeendelea kwa utulivu kwa muda mrefu, na China imezisaidia nchi za Afrika kuendeleza uchumi, kuimarisha uhuru, na kutatua masuala ya kijamii. Ameongeza kuwa anatarajia kuimarisha ushirikiano na China ili kupata mafanikio ya pamoja.