Tibet yafanikisha kufikia lengo la uwiano wa kaboni
2023-09-11 10:44:08| CRI

Mkuu wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet uliopo Kusini magharibi mwa China Yan Jinhai, amesema mkoa wake umefanikisha uwiano wa kaboni kwa ujumla na unaweza kutoa mchango mkubwa zaidi katika malengo mawili ya hewa ya kaboni ya China.

Hayo ameyasema kwenye Kongamano la Namjagbarwa kuhusu kujenga uwanda wa juu wenye ustaarabu wa ikolojia huko Tibet lililofunguliwa jana Jumapili katika mji wa Nyingchi wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa wataalam waliohudhuria kongamano hilo hivi sasa hewa ya kaboni inayoshuka kwenye mfumo wa ikolojia wa Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet ni tani milioni 162 kwa mwaka, ikichukua asilimia 8 hadi 16 ya jumla ya hewa ya kaboni inayoshuka ya mfumo wa ikolojia wa China.

Zaidi ya maafisa 120 wa serikali, wataalamu na wasomi wakiwemo wanataaluma maarufu kutoka Chuo cha Sayansi cha China na Chuo cha Uhandisi cha China wako kwenye kongamano hilo la siku mbili.