Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco yafikia 2,122
2023-09-11 13:45:45| cri

Watu 2122 wamefariki na wengine 2,421 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katikati ya Morocco ijumaa usiku.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, watu 1,351 walifariki katika mkoa wa Al Haouz, 492 mkoani Taroudant, 201 mkoa wa Chichaona na 17 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Marrakesh.

Vikosi vya usalama na huduma za dharura nchini humo vinajitahidi kufikia maeneo yaliyoathiriwa zaidi katika Milima ya Atlas, kutokana na barabara zinazokwenda sehemu hiyo kuzibwa na majabali yaliyoanguka.

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Afya Duniani (WHO), janga hilo limeathiri zaidi ya watu 300,000 katika mji wa Marrakesh na miji jirani.