Africa CDC kushirikiana na nchi wanachama wa Kundi la G20 juu ya masuala ya afya
2023-09-11 10:49:53| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Jumamosi kilisema kitashirikiana na nchi wanachama wa Kundi la G20 juu ya masuala ya afya.

Africa CDC ambayo ni shirika maalumu la matibabu la Umoja wa Afrika (AU) imepongeza uamuzi wa kuipatia AU uanachama wa kudumu katika Kundi la G20. Africa CDC ilisema maendeleo hayo yanaashiria kuwa Afrika imekuwa mshiriki muhimu kwenye jukwaa la dunia, na iko tayari kushughulikia masuala ya bara hilo ambalo ni eneo kubwa zaidi la biashara huria kote duniani. Afrika CDC itashiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa afya wa Kundi la G20 kwa niaba ya nchi za Afrika.

Wakati huohuo Umoja wa Nchi za Kiarabu (AL) Jumapili ulipongeza uamuzi wa kuipatia AU uanachama wa kudumu katika Kundi la G20, ukisema AL nayo inatumai itapata nafasi kama hiyo.