Misri yasema hatua ya Ethiopia ya kujaza maji kwenye bwawa la Nile ni ukiukaji wa makubaliano ya pande tatu
2023-09-11 10:45:20| CRI

Misri kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje imesema hatua ya Ethiopia ya kujaza maji kwenye bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) bila kukubaliana na Misri na Sudan, ni ukiukaji wa Azimio la Kanuni, ambalo ni makubaliano ya pande tatu yaliyosainiwa mwaka 2015.

Jumapili, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, kukamilika kwa duru ya nne na ya mwisho ya kujaza maji kwenye bwawa la GERD.

Azimio la Kanuni linasema kuwa nchi hizo tatu lazima zikubaliane juu ya sheria za kujaza na kuendesha GERD kabla ya kuanza mchakato wa kujaza. Imeongeza kuwa, kuchukua hatua hizo za upande mmoja ni kutojali maslahi na haki za nchi zinazopitiwa na mto huo na usalama wao wa maji chini ya sheria za kimataifa.