Kenya yazindua jukwaa la kidijitali kwa uwekezaji katika dhamana za serikali
2023-09-12 23:31:38| cri

Rais wa Kenya William Ruto jana jumatatu amezindua jukwaa la kidijitali linalowezesha uwekezaji katika dhamana za serikali.

Rais Ruto amesema miundombinu ya Kituo Kikuu cha Uwekezaji wa Dhamana (CSD) kilicho chini ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kinawezesha uuzaji wa dhamana za serikali kupitia majukwaa ya moja kwa moja mtandaoni na kwenye simu za mkononi. Amesema jukwaa hilo la kidijitali linaondoa haja ya wawekezaji kwenda wenyewe katika Benki Kuu ya Kenya ili kununua dhamana za serikali, na pia litawezesha wakenya wanaoishi nje ya nchi kununua dhamana hizo.

Rais Ruto pia amesema, jukwaa hilo litaimarisha soko la mitaji la ndani, na kuboresha uwekezaji na utunzaji wa akiba.