Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco yazidi 2,600
2023-09-12 10:17:10| CRI

Taarifa mpya iliyotolewa Jumatatu na serikali ya Morocco ilisema idadi ya vifo nchini humo kutokana na tetemeko kubwa la ardhi imeongezeka hadi 2,681, na idadi ya majeruhi imefikia 2,501.

Vikosi vya uokoaji vilivyotumwa na Hispania na Uingereza vimefika kijiji cha Amizmiz kilichoko karibu na kitovu cha tetemeko hilo. Helikopta zilionekana zikienda na kurudi kati ya mji mkongwe wa Marrakesh ulioathirika zaidi na sehemu nyingine zilizokumbwa na tetemeko la ardhi.

Kazi za uokoaji pia zinaendelea kufanyika ili kuweza kuingia maeneo ya mlimani yaliyoathiriwa vibaya zaidi kwenye tetemeko hilo.