Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini aondoka kuelekea Russia
2023-09-12 10:20:54| CRI

Shirika la Habari la taifa la Korea limesema kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini ambaye pia ni rais wa nchi hiyo Kim Jong-Un aliondoka Jumapili mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pyongyang kwa treni na kwenda kwenye ziara yake nchini Russia.