Umoja wa Afrika watoa salamu za rambirambi kwa Libya kufuatia maafa ya mafuriko
2023-09-13 23:09:33| cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa salamu za rambirambi kwa Libya kufuatia maafa ya mafuriko yaliyotokea nchini humo.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii wa X, Bw. Mahamat ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuisaidia Libya kukabiliana na maafa hayo.

Watu 5000 wamefariki mashariki mwa Libya kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel mwishoni mwa wiki iliyopita, na mamlaka za huko zimetangaza siku tatu za maombolezo kuwakumbuka watu waliofariki kutokana na mafuriko hayo.