Kenya yaanza marekebisho ili kuongeza mapato ya kodi hadi asilimia 25 ya Pato la Taifa
2023-09-13 09:51:08| CRI

Serikali ya Kenya Jumanne ilitangaza mkakati wa marekebisho ya kodi ambayo inataka kutumia ili kuongeza mapato katika miaka ya fedha ya 2024/2025 na 2026/2027 na katika kipindi cha kati.

Akielezea kuhusu waraka huo uliopewa jina la Mkakati wa Mapato ya Muda wa Kati, Waziri wa Hazina ya Kitaifa Njuguna Ndung'u, amesema serikali itatumia marekebisho hayo kuongeza mapato hadi asilimia 25 ya pato la taifa (GDP). Alibainisha kuwa mavuno ya mapato ya Kenya bado yako chini ya lengo linalotarajiwa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) la asilimia 25 ya Pato la Taifa, hivyo mkakati huu unaainisha marekebisho ya mfumo wa kodi yenye lengo la kurudisha nyuma mwelekeo wa uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa na kufikia uwiano wa asilimia 25 kwa mwaka hadi 2030.

Baadhi ya marekebisho yaliyopendekezwa ni pamoja na mapitio ya kodi ya bidhaa za petroli, faida iliyorejeshwa, tumbaku na vileo pamoja na kuanzishwa kwa kodi ya bidhaa za makaa ya mawe.