Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini awasili Russia katika mji wa mpakani Khasan
2023-09-13 09:49:34| CRI

Shirika Kuu la Habari la Korea (KCNA) limeripoti kuwa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amewasili Russia katika mji wa mpakani wa Khasan mapema Jumanne, ambapo yupo nchini humo kwenye ziara rasmi ili kuweka uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Russia katika kiwango kipya cha juu.

Treni binafsi ya Kim iliingia kwenye Kituo cha Reli cha Khasan saa 12 asubuhi kwa saa za huko. Wakati wa mazungumzo yake na maafisa wa Russia katika chumba cha mapokezi cha kituo cha reli, Kim alisema kuwa ziara hiyo nchini Russia, ambayo ni ya kwanza ya nchi za nje tangu janga la COVID-19, ni dhihirisho wazi la msimamo wa chama tawala na serikali ya Korea Kaskazini, ikitoa kipaumbele umuhimu wa kimkakati wa uhusiano kati ya pande hizo mbili.