Ushirikiano wa Kusini na Kusini una uwezo mkubwa wa kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa
2023-09-13 09:47:02| CRI

Ushirikiano wa Kusini na Kusini una uwezo mkubwa wa kusaidia nchi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Hayo yalisemwa na wajumbe waliokuwa wakizungumza katika shughuli iliyofanyika mjini Kigali, Rwanda ya kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano wa Kusini na Kusini, ambayo hufanyika Septemba 12 kila mwaka.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Rwanda Manasseh Nshuti alitoa wito katika hafla hiyo kuwa kila mmoja anapaswa kutafakari uwezo mkubwa ulio nao ushirikiano wa Kusini na Kusini, na sio tu katika kubadilishana mawazo au kusaini mikataba, bali ni kuunda mshikamano wa kudumu ambao utainua nchi za Kusini na kubadilisha mustakabali wa pamoja.

Ameeleza imani yake kuwa ushirikiano wa Kusini na Kusini una uwezo mkubwa wa kufungua fursa za nchi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs, kupitia kutumia nguvu ya ushirikiano na kusaidiana na kuboresha maisha ya watu.