Jeshi la Kenya lawaua wapiganaji watano wa kundi la Al-Shabaab
2023-09-14 23:40:31| cri

Jeshi la Kenya limewaua wapiganaji watano wa kundi la Al-Shabaab na kukamata vifaa vinavyotumika kutengeneza mabomu ya kienyeji (IED), dawa na vifaa vingine katika msako uliofanyika mapema jumatatu katika eneo la Harbole-Fasi ambalo ni maficho ya wapiganaji hao.

Kikosi maalum cha jeshi kilichopata taarifa za kiintelijensia kilivamia eneo hilo linaloaminika kuwa kambi ya ugavi ya kundi hilo la kigaidi. Inaaminika kuwa kambi hiyo ilitumika kutengeneza na kutega mabomu yaliyotengenezwa kienyeji katika njia kuu za ugavi ndani ya kaunti ya Garissa na kaunti ya jirani ya Lamu, ambayo imeshuhudia ongezeko la mashambulio ya mabomu yakilenga raia wa kawaida na maofisa wa usalama.