Xi na Maduro watangaza kuinua uhusiano kati ya China na Venezuela
2023-09-14 09:54:47| CRI

Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na mwenzake wa Venezuela, Nicolas Maduro Moros, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Umma jana Jumatano, ambapo walitangaza kuinua uhusiano kati ya China na Venezuela na kuwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote.

Rais Xi alisema kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote kati ya China na Venezuela kunakidhi matarajio ya pamoja ya watu wote wa pande mbili na kuendana na mwelekeo wa jumla wa maendeleo ya kihistoria, na kutoa wito kwa pande hizo mbili kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati utakaozaa matunda zaidi kati ya China na Venezuela, kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande mbili na kuwa chachu zaidi katika amani na maendeleo ya dunia.

Akizungumzia mageuzi na ufunguaji mlango wa China, hususan maendeleo ya maeneo maalum ya kiuchumi rais Xi alibainisha kuwa mageuzi na ufunguaji mlango ni nyenzo muhimu kwa China ya kuendana na wakati kwa hatua kubwa na muhimu katika kuifanya China kuwa kama ilivyo leo.

Kwa upande wa Maduro alisema maendeleo ya Venezuela na uhusiano baina ya Venezuela na China upo katika hatua muhimu, na kwamba kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote ina umuhimu wa kihistoria na kwa hakika utaleta enzi mpya ya mahusiano baina ya nchi mbili.