Watu 40 wauawa mkoani Darfur nchini Sudan
2023-09-14 14:41:07| cri

Watu 40 wameuawa katika shambulio la anga mkoani Darfur jana jumatano, wakati kiongozi wa jeshi la nchi hiyo Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan akielekea nchini Uturuki.

Watu walioshuhudia shambulio hilo wamesema, shambulio hilo limetokea katika masoko mawili na kusababisha maafa makubwa kwa raia katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Sudan, ambako mashambulio yameongezeka katika mwezi mmoja uliopita.