Watalii kutoka Afrika ni kichocheo katika ufufukaji wa sekta ya utalii nchini Kenya
2023-09-14 09:59:18| CRI

Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Urithi wa Kenya Peninah Malonza Jumatano alisema kutokana na kupanuka kwa safari za kikanda, watalii kutoka Afrika wamekuwa kichocheo cha ufufukaji wa sekta ya utalii nchini Kenya.

Malonza alisema Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria na Ghana zimekuwa chanzo muhimu cha masoko ya sekta ya utalii ya Kenya. Akizungumza na wanahabari juu ya Maonyesho ya tatu ya utalii wa Afrika Mashariki yatakayofanyika tarehe 20 hadi 22 Novemba nchini Kenya, Malonza alisema utendaji wa nchi za Afrika ni ushahidi tosha kuwa kuna uwezo mkubwa ambao haujaguswa huko Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, sekta ya utalii ni moja ya vyanzo vikuu vya fedha za kigeni kwa Kenya pamoja na upelekaji fedha kutoka diaspora, kilimo cha bustani na uuzaji wa chai nje.