Russia na Korea Kaskazini kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema na kukuza amani ya kikanda
2023-09-14 09:56:07| CRI

Russia na Korea Kaskazini zitajitahidi kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema na kukuza amani ya kikanda.

Hayo yamesemwa na rais Vladimir Putin wa Russia alipokutana na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jana Jumatano katika ukumbi wa Vostochny Cosmodrome. Akikumbushia kwamba Umoja wa Kisovyeti ulikuwa wa kwanza kutambua mamlaka na uhuru wa Korea Kaskazini, Putin alisema wameazimia kuimarisha uhusiano wao wa urafiki na ujirani mwema, na kuongeza kuwa nchi zote mbili zitachukua hatua kwa jina la amani, utulivu na ustawi.

Kwa upande wake, Kim alibainisha kuwa ziara yake inafanyika wakati wa makabiliano makali katika uga wa kimataifa, makabiliano kati ya maendeleo na mwitikio, haki na ukosefu wa haki, huku kukiwa na ulimwengu mpya unaoibukia wa pande nyingi.

Kim alisema amejadili hali ya kijeshi na kisiasa katika Peninsula ya Korea na bara la Ulaya na mwenzake wa Russia, na kuongeza kuwa pande zote mbili zimekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kimbinu.