China yatoa wito wa kuondoa vikwazo vya upande mmoja ili kuboresha kazi za kibinadamu
2023-09-15 09:44:34| CRI

Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun ametoa wito wa kuondoa vikwazo haramu vya upande mmoja ili kuboresha kazi ya kimataifa ya kibinadamu.

Wito huo ameutoa kwenye Baraza la Usalama la mjadala wa wazi juu ya kuendeleza ushirikiano wa kibinadamu wa sekta ya umma na binafsi. Bw. Zhang aliendelea kufafanua kuwa vikwazo haramu vya upande mmoja vinaathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa sekta ya umma ya nchi husika kutoa huduma za msingi kama vile elimu na usambazaji wa chakula, na kuingilia shughuli za kawaida za sekta binafsi katika biashara, uwekezaji na uendeshaji biashara, na hivyo kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa ushirikiano wa kibinadamu na umma na binafsi.

Alisisitiza kuwa Jumuiya ya kimataifa inapaswa kwa pamoja kuzihimiza nchi zinazohusika kuondoa mara moja vikwazo vya upande mmoja, kuondoa athari zake mbaya, na kuunda mazingira mazuri kwa shughuli za kibinadamu za kimataifa.